THE
MILLIONAIRE CODE
MAMBO
20 NILIYOJIFUNZA KUTOKA KITABU CHA THE MILLIONEIRE CODE BY PAUL B. FARRELL.
Si kila mtu amezaliwa na asili
ya kuweka akiba , na kuwekeza na kuwa na Mafanikio wengine mafanikio kwao si alama ya fedha ,
Cheo , Nafasi ya juu._
Mwanagenzi Michael The Great
one.
__________________________________________________________________
Mwandishi anaibua jambo la
ajabu sana ambalo wengi wetu limekuwa jambo linalotuzuia kuyafikia mafanikio
tuyatakayo, nalo si jingine bali ni kufikiri kuwa njia aliyoitumia yule na
kupata mafanikio yaweza kukutoshea na wewe kuwa mwenye mafanikio, jambo ambalo
ni uongo na wengi limewafanya kufanya maamuzi ya hovyo ya kiuwekezaji na
kushindwa kwa kukata tamaa na kuishia njiani.
Kitabu hiki bora kinakuja na
msingi mkuu wa wewe pia kufanya maamuzi ya kuelekea utajiri wako kulingana na
kutokana njia yako inayokufaa.
1. Jambo
muhimu kwenye mafanikio yoyote unayoyataka, ni kwa kuanza kwanza kujitafuta
wewe na kujifahamu na ukisha jifahamu vyema utaona mwili wako unafuata matendo
ya kutengeneza utajiri bila kuchoka ama kukata tamaa.
2. Unahitaji
kukua sana kihisia ili uwe na uwezo wa kujitawala kihisia ,hapo ndiyo utakuwa
kwenye mwelekeo wa njia nyoofu, udhaifu wa kutawala hisia zetu ndiyo jambo
linalowatumbukiza wengi kwenye umaskini.
3. Furaha
na mafanikio yapo kwenye ngazi ya kujifahamu wewe na huko utakuwa na funguoa za
kujifungua yaani (Codes) zako , ili kuchukua njia sahihi inayokufaa.
4. Ugumu
wa jambo la ya kuyafikia mafanikio haupo kwenye kuanza jambo fulani, bali tatizo
kubwa lipo kwenye kufahamu njia sahihi ya kuiendea , maana unaweza kuanza na
njia mbovu isiyokuwa yako na ukaja kugundua muda umeshakwenda.
5. Pamoja
na wataalamu wengi kufundisha njia na mbinu mbalimbali za kupata mafanikio lakini bado kiwango cha
chini cha matajiri yaani watu wanne kati ya watu milioni mia mbili , tatizo ni
kuwa ushauri unaotolewa wataalamu wanafikiri kuwa kila mmoja utamfaa jambo
ambalo si kweli. Vyema kutafuta njia na ushauri unaoendana na wewe ili ukufae.
6. Epuka
mtego wa kuwa na taarifa zilizopitiliza kuhusiana na mwelekeo wa kuwa tajiri,
kuwa na taarifa zilizo nyingi bila kufahamu ipi inafanya kazi kwa usahihi ni
sawa na kazi bure.
7. Epukana
na tabia ya kuyakubali na kujifunza mambo unayoyafahamu tu na yale usiyoyajua
unayaacha na kuyapuuza huko ndiko kunakokuzuia kufanya mabadiliko muhimu kwenye
maisha yako.
8. Asilimia
90% ya watu wanaofanya maamuzi ya kufanya uwekezaji hufanya uwekezaji kwa njia
zisizo sahihi kabisa na hubaki kwenye majuto ya daima.
9. Makampuni
mengi yanayowashawishi watu kufanya uwekezaji kwenye eneo fulani, mengi hutumia
gharama za juu sana za matangazo na kuwahadaa watu ili yajipatie fedha zao na
kutajirika.
10.
Mara zote usiogope kuwa wa tofauti na kubali
kuwa wewe ni wa kitofauti kabisa, fanya mambo yako kwa utofauti kwakua kila
kitu kwako ni cha kitofauti kama:-
a)
Gene
b) Vinasaba
c)
Na njia yako pia itakuwa ya kitofauti.
11.Kujifahamu
na kujijua wewe ndiyo jambo lililoandikwa kwa miaka mingi sana zaidi ya miaka
elfu tano iliyopita na ndugu wa Lao Tzu kwenye kitabu chake cha Tao Te Ching,
na limelejewa na wanafalsafa wakubwa kama Plato aliyesema Know Thyself , basi
na kwako pia jifahamu, wewe na kuwa wewe.
12.
Kama unapata wakati mgumu , jifunze kujisikiliza
ndani yako kuna sauti inayokwambia wewe ulivyo , sikiliza kwa umakini mzuri.
13.
Anza leo kukaa darasani , ujifunze kuwa milionea
na kutafuta Njia yako ya kuelekea utajiri wako na hakikisha unayapuuza haya:-
a) Usiwasikilize
wengine wanasemaje kukusu wewe?
b) Usikazie
fikra kwenye kazi ya miaka mingi uliyofanya.
14.
Fanya mabadiliko makubwa kwenye maisha yako ili
usiishie kwenye aina ya maisha haya:-
i)Maisha
yenye furaha bila fedha za kutosha.
ii)Maisha
yasiyo na furaha bila fedha.
iii)Maisha
yasiyo na furaha na una fedha.
15.
Ili kushika usukani wa Maisha yako , ondoa
visababu, na hapo utaona mambo yakitimia , wacha kujiambia Mimi sina msaada.
16.
Hatua za mafanikio huja pale , unapoamua
kubadilika , bila kubadilika utajichelewesha wewe mwenyewe.
17.
Hizi ndiyo njia ambazo huwa unatumia kufanya
maamuzi yako mbalimbali kwenye Maisha yako kuwa Nazi umakini:-
i)Hisi
(Sensation) hizi husema kitu kipo
ii)Kufikiri
(Thinking) (husema kitu kilivyo.
iii)Hisia
(Feeling) hizi huwa zinasema unakubali au la
iv)Machale
(Intuition), hii inasema wakati wa kuja.
18.
Umba ubongo wako uwe wa kiuwekezaji kama unataka
kuwa mwekezaji bora na wa juu na uwe na ubongo wa (neuroeconomic)
19.
Jifunze kuwa na wazo moja na lengo moja na huko
mimina uwezo wako wote.
20.
Goma
kuishi Maisha ya ukawaida wewe si wakawaida nenda viwango vya juuu vya upekee
wako.