Home Ads

   SAFARI YA UTAJIRI NA NJIA ZAKE KUTOKA KITABUNI

 

U

TAJIRI ni SAFARI inayopitishwa katika hatua hizi 22 ambazo Mwandishi David Gikandi anaelezea kupitia kitabu chake cha "A HAPPY POCKET FULL of MONEY"

Utajiri ni utambuzi wa fikra kwanza kabla ya kupatikanika. Wale wanaotambua hili basi huanza na kubadili kufikiri kwao kisha utajiri unaweza kuvutwa kirahisi. Fedha ni sehemu tu ya aina za utajiri ambazo watu wengi wanajua. Lakini kuna aina za utajiri mbali na fedha ambazo si wengi wana utambuzi huu. Karibu tuone hatua 22 za safari ya kutambua utajiri na maisha ya furaha.

1.     Kwanza kabisa lazima utambue wale ambao wanaweza kufanya makubwa maishani huwa wana utambuzi wa namna Dunia ifanyavyo kazi au vitu vinavyofanya kazi. Kisha kwa kujua huko wanaendana na huo mfumo wa mambo ulivyo. Utambuzi wa Dunia inavyofanya kazi ni maarifa makubwa ambayo yamefanya watu wengi waje na ugunduzi, ubunifu na kutengeneza utajiri mkubwa tofauti na wale wasio na utambuzi huo.

 

2.   Ufahamu wa muda unatenganisha watu katika kuyaelewa maisha. Muda ni kiinimacho kwa watu wengi. Ukiondoa fikra basi umeondoa uwepo wa muda. Hivyo muda pekee ambao ni halisi ni sasa. Kwa wanaopanga malengo basi kwa kujua hili hupanga malengo yao kama yameshakuwa sasa.


3.   Maisha ni ujenzi wa picha akilini mwa mtu. Fikra na hisia za mtu zinapoumba picha ndivyo mtu anavyovuta maisha yaliyo sawa na picha anazoruhusu ziwe katika fikra zake.

 

4.   Kufikiri huzalisha mawazo na mawazo ni nguvu yenye umbo. Mara ngapi jambo uliwaza halafu baada ya muda likatokea ?. Basi hii ndiyo nguvu ya uvutano ya mawazo na kutokea kwa kitu katika umbo. Wenye utambuzi huu hudhibiti mawazo yao wakijua mawazo ni maumbo yanayoweza kutokea.

 

5.    Watu wengi hawana ufahamu wa kina wa kupanga malengo yanayoendana sawa na Dunia inavyofanya kazi na hivyo kujikuta hawapati matokeo sawa na malengo yao. Wenye utambuzi wa kuyahusianisha malengo na ulimwengu unavyofanya kazi basi huwa wanapata matokeo wanayoyataka.

 

6.   Ili uweze kuumba kitu lazima kwanza uruhusu uwe ( State of being ). Ili upate utajiri lazima kwanza ujione ndani yako utajiri kisha uchukue hatua za malengo ya kukufanya uwe utajiri kisha upate utajiri kwa kuuona katika umbo. ( Formula ni kuwa, kufanya na kupata ). Lazima upitie ( TO, BE & HAVE ). Ila wengi hupuuza hii formula ndo maana kutengeneza maisha mazuri au utajiri ni safari ngumu kwao.

 

7.    Bila kuchukua hatua huwezi kupata ulichokifikiri. Kuchukua hatua ni kuruhusu kitu kiweze kutokea. Hata kama utafikiri vizuri, utapata malengo vizuri na ukakosa kuchukua hatua hakuna utakachokipata.

8.   Lazima uwe na utambuzi kuwa ulimwengu una utele kuliko uhaba. Uhaba ni vile fikra zako zilivyo.


9.   Sheria ya asili ya kupanda na kuvuna kadri unavyoweza kuitambua utakuwa unajua namna ya kutengeneza matokeo utakayo kwa kuangalia upande nini ili uvune nini. Hii ni sheria mama ya kutengeneza utajiri na maisha ambayo ungependa yawe kwa uzuri.
 
10.                    Kuna watu hukosea pale wanapoangalia utajiri kuwa una mazingira fulani pasipo kujua ni kitu kinachotengenezwa tokea ndani.


11.Mafanikio na kufeli ni pande moja ya shilingi. Kufeli ndio njia ya kujua usahihi wa jambo na ukafanikiwa. Wenye utambuzi huu basi huona kila hatua ya kufanikiwa kwao kufeli ni sehemu ya mafanikio

12.                     Kuna vitu ambavyo huangusha watu kuwa na utajiri na furaha. Na hili lazima uliepuke ( ndani ya kitabu hiki tutajifunza namna ya kufanya hivyo )


13.                     Swali la nini kusudi la maisha yangu ? Nipo naishi ili iweje ni muhimu sana kujiuliza. Kitabu hiki kimejibu vizuri kiasi cha kushibisha kiu yako.

14.                     Utoaji ni njia ya utajiri. Wenye utambuzi huu wanajua ili ufanikiwe na kujifahamu wewe ulivyo basi kwa njia ya kujitoa kuanzia vipaji, muda wako ndivyo utakavyoweza kujifahamu zaidi.

15.                     Watu wengi wanadharau nguvu iliyopo katika kushukuru. Kushukuru kuna Nguvu kubwa ya kuvuta maisha bora.

16.                     Utambuzi ( Consciousness ) ndio kikwazo cha watu wengi washindwe kupata baadhi ya vitu maishani hata kama vipo. Kadri unavyokua ki utambuzi utaona Dunia ina utele na sio uhaba.

17.                     Wewe ni mjenzi wa kwanza wa maisha ulonayo. Wewe ni kisababishi cha matokeo unayoyapata nje. Kama hivyo maisha mazuri na mabaya yapo kwako mtengenezaji.

18.                    Kila kitu kinahusiana na vyote ni kama katika umoja. Wale wanaojua hili basi wanatambua namna kwa jambo dogo linaweza kuumba makubwa.

19.                     Dunia ni tele na wewe ni sehemu ya utele. Ndani yako kuna uwezo usioweza kupimwa ukaisha.

20.                   Ili ufanikiwe na kuwa na furaha lazima urejee katika asili yako na hapo ndipo chimbuko la furaha na utajiri wako.

21.                     Fedha ni kiinimacho na ijue fedha halisi ni ipi itakupa hatua za juu sana katika maisha.

22.                   Unapojua haya basi wasaidie wengine kujua na uwafundishe kujua ndivyo utajiri unavyoweza kusambaa kwa wengi.

Huu ni mwanzo wa safari ya kitabu hiki. Hakika hutakuwa ulivyokuwa. Hebu chukulia uzito katika haya na maisha yako hayatakuwa yalivyokuwa.

 

Author

Contact Us

Name

Email *

Message *